October 25, 2020

KISINDA AAHIDI MAKUBWA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Winga wa Yanga,Tuisila Kisinda amesema kuwa anajiona  bado hajacheza katika kiwango chake cha juu  lakini atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha anatoa mchango mkubwa kwa timu kuhakikisha inafanya vizuri katika michezo ijayo ya Ligi.

Yanga katika mchezo unaofuta wa ligi inatarajiwa kumenyana na Mtibwa Sugar Jumapili, Septemba 27 katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kisinda amejiunga na Yanga akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo ambapo tangia ajiunge na timu hiyo amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

Kisinda amesema kuwa bado hajacheza na kufikia katika kiwango chake cha juu  lakini atajitahidi kuhakikisha anatimiza majukumu ya Yanga kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya ligi kuu.

“Mashabiki wanatakiwa kuwa na subira lakini waendelee kuiunga mkono timu yao,kwa upande wangu  bado sijacheza katika kiwango kizuri lakini naamini  huko mbeleni kwenye michezo ijayo natarajia kuona mambo yakiwa mazuri.

“Kuhusu ligi ya Tanzania Kuna mambo najifunza kupitia ligi hii ambayo nimegundua kuwa inawachezaji wengi wazuri na ina ushindani mkubwa hivyo inahitaji kupambana ili kupata matokeo na mimi nipo tayari kwa hilo,” amesema Kisinda

1 thought on “KISINDA AAHIDI MAKUBWA YANGA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *