October 28, 2020

MWAISABULA AIPA USHAURI YANGA KUMPATA NAHODHA

Msomaji wa Yanganews Blog: Kocha wa zamani wa Yanga, Kennedy Mwaisabula amesema ili mtu awe nahodha wa timu ni lazima awe na sifa zifuatavyo, kuwa kiongozi na kusikilizwa na wenzake mwenye kuunganisha wachezaji na viongozi na kuchuja anachokiwasilisha, usupa staa ndani ya timu, kupata nafasi ya kucheza kikosini mbali na kuitumikia timu kwa muda mrefu na kujua miiko na tamaduni zake.

“Ni lazima mchezaji awe na sifa hizo, ndio maana mara nyingi manahodha wanakuwa na mastaa wa timu, yaani wenye ushawishi na kusikilizwa, pia mwenye nafasi kikosini, kwangu ningetakiwa kuteua mmoja, basi Niyonzima angefaa zaidi, ila Kocha Zlatko ndiye mwenye uamuzi wa mwisho,” alisema Mwaisabula.

3 thoughts on “MWAISABULA AIPA USHAURI YANGA KUMPATA NAHODHA

  1. viongozi swala la tiketi uwanja wa mkapa ni changamoto siku ile ya mechi ya ufunguzi watu wengi waliludi majumbani kwasababu watoaui tiketi bi wachahe mimi nilipata nafasi ya kuingia kipindi cha kwanza kimeisha wakati nilifika getini saa 11 mlikemee hilo lisitokee tena kwani wanatukatisha tamaa ya kwenda uwanjani mimi ninae ongea usumbufu wa tiketi kuhangaishwa mpaka nilipata hasala ya kupoteza simu yenye thamani ya laki mbili na sabini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *