October 28, 2020

ALICHOSEMA MANEJA YANGA KUELEKEA MECHI LIGI KUU DHIDI MTIBWA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, ameliambia chanzo chetu kuwa wamefika salama na wanatarajia kuendelea na maandalizi ya mechi hiyo wakiwa na wachezaji wao wote.

Hafidh alisema kila mchezaji yuko tayari kuikabili Mtibwa Sugar na wanajua wapinzani wao wamejipanga kutopoteza pointi kwa mara nyingine.

“Tumeshafika Morogoro, tunajua upinzani utakuwapo, Mtibwa Sugar si timu ndogo, tumewaangalia mechi zao zilizopita na kujua uwezo wa kila mchezaji, hatutazubaa, tutaongeza umakini wakati wote wa mchezo,” alisema meneja huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *