October 20, 2020

TONOMBE APELEKA KILIO KAITABA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kikosi cha Yanga SC imeweza kuitungua Kagera Sugar kwa kuwachapa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mserbia, Zlatko Krmpotic inafikisha pointi saba baada ya mechi tatu, ikishinda mbili na sare moja katika mechi zake mbili za awali nyumbani, Dar es Salaam.

Kwenye mchezo huo uliochezeshwa na refa Hussein Hamisi wa Katavi aliyesaidiwa na Joseph Masija wa Mwanza na Robart Rwemeja wa Mara, bao pekee la Yanga SC limefungwa na kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Serge Mukoko Tonombe.

Tonombe alifunga bao hilo dakika ya 73 baada ya kutuliza vizuri mpira kwenye boksi na kumchambua kipa Issa Chalamanda kwa shuti la juu kufuatia pasi ya mchezaji mwenzake wa zamani wa AS Vita ya Kinshasa, kwaoDRC.

Kikosi cha Yanga kilikuwa; Metacha Mnata, Kibwana Shomari/Deus Kaseke dk57, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Zawadi Mauya/Harouna Niyonzima dk80, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Michael Sarpong, Yacouba Sogne/Carlos Calinhos dk57 na Tuisila Kisinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *