October 28, 2020

REKODI ZAIBEBA YANGA, MECHI DHIDI KAGERA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Kikosi cha Yanga itakuwa ugenini leo Jumamosi kucheza mechi yake ya kwanza ugenini dhidi ya Kagera Sugar.

Licha ya nyota wake wapya kama Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Michael Sarpong, Yacouba Sogne na Carlinhos ambao kwa mara ya kwanza watacheza kwenye Uwanja wa Kaitaba, rekodi za misimu mitano ya Ligi zinaibeba Yanga.

Katika misimu mitano, Yanga imeifunga Kagera mara tisa, huku kipigo kikubwa zaidi kuiadhibu timu hiyo Kaitaba kikiwa cha mabao 6-2 Oktoba 22, 2016.

Kagera yenyewe katika misimu mitano, imeifunga Yanga mara moja Jan 3, 2020.

Oktoba 31, 2015, Kagera ikicheza nyumbani ilikubali kipigo cha mabao 2-0, kabla ya kuendeleza uteja kwa Yanga Aprili 2, 2016 kwa kipigo cha mabao 3-1, Dar es Salaam.

Oktoba Oktoba 22, 2016, Kagera iliduwazwa na Yanga kwa kipigo cha mabao 6-2 mjini Bukoba na Aprili 13, 2017 ikaruhusu kipigo kingine cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa marudiano.

Oktoba kwa mara ya tatu uliendelea kuwa mchungu kwa Kagera Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani, ambapo Oktoba 13, 2017 waliruhusu kipigo kingine cha mabao 2-1 na Machi 7, 2018 wakafa Taifa kwa mabao 3-0.

Msimu wa 2018/2019, Kagera tena ilianza kwa kipigo cha mabao 2-1 nyumbani Agosti 25, 2018 na kipigo kingine cha mabao 3-2 Januari 8,2019 jijini Dar es Salaam.

Kagera iliwafunga Wananchi msimu wa 2019/2020 baada kuwafunga mabao 3-0 Januari 3, 2020 kwenye Uwanja wa Mkapa, hata hivyo Yanga iliitundika bao 1-0 kwenye mchezo wa marudiano mjini Bukoba Julai 8.

Msimu mpya wa Ligi pia rekodi inaibeba zaidi Yanga ambayo ina pointi nne katika mechi mbili ilizokwishacheza, imetoka sare moja na kushinda moja.

Kagera yenyewe imefungwa mechi moja na kutoka sare moja ikiwa na pointi moja katika mechi mbili.

Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic, raia wa Serbia amesisitiza kutaka pointi tatu katika mchezo huo; “Tunaamini tutafanya vizuri, tuna ari na morali ya ushindi na kuchukua pointi tatu na kuanza vizuri mechi yetu ya kwanza ugenini.”

1 thought on “REKODI ZAIBEBA YANGA, MECHI DHIDI KAGERA SUGAR

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *