October 28, 2020

WACHEZAJI YANGA MZUKA UMEPANDA, KAGERA SUGAR WAMEKWISHAA

Msomaji wa Yanganews Blog:Leo patachimbika dimba la Kaitaba, ambako kikosi cha mabingwa wa kihistoria Yanga itashuka dimbani kumenyana dhidi ya Kagera Sugar huo ukiwa mchezo wa ligi kuu, utakopigwa saa10jioni.

Hafidh Saleh, akizungumzia maandalizi ya timu hiyo, alisema wamesafiri na jumla ya wachezaji 20 na wote wapo tayari kwa mchezo huo, hivyo ni jukumu la kocha kuamua aanze na nani.

Saleh alisema wanatarajia utakuwa mchezo mgumu kwa pande zote, lakini wamejipanga kuvuna pointi tatu kwa kuwa lengo lao msimu huu ni kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

“Kagera Sugar si timu ya kuibeza hata kidogo, tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tumefanya maandalizi mazuri na wachezaji wote wapo fiti kwa mchezo na wana ari ya kufanya vizuri, tusubiri tuone,” alisema meneja huyo.

Kuhusu majeruhi, meneja huyo alisema mbali na Mapinduzi Balama, wachezaji wote wapo fiti na wale ambao hawakusafiri na timu, wanaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam.

Yanga ambayo ilitua mjini hapa kwa ndege juzi saa 3:30 asubuhi, tangu ametua kiungo wa timu hiyo, raia wa Angola, Carlos Carlinhos ndilo jina ambalo limekuwa likitajwa na kusifiwa zaidi na mashabiki wa timu hiyo mjini hapa.

Kila mmoja amekuwa akitamani kuona akianzishwa katika kikosi cha kwanza kitakachoanza leo, lakini bado uamuzi huo unabaki chini ya Zlatko ambaye awali aliliambia chanzo chetu kuwa mchezaji huyo bado hajawa fiti kutosha kucheza kwa dakika zote 90 za mchezo, hivyo ataendelea kupata muda mchache dimbani sambamba na mshambuliaji, Sogne Yacouba, raia wa Burkina Faso.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema: “Msimu huu tumesajili vizuri na tunamatumaini ya kushinda kwa kuwa lengo letu msimu huu ni kutwaa ubingwa.”
Wachezaji wa Yanga ambao hawakusafiri na timu mbali na Balama ni pamoja na Paul Godfrey, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na kipa Farouk Shikalo.

1 thought on “WACHEZAJI YANGA MZUKA UMEPANDA, KAGERA SUGAR WAMEKWISHAA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *