October 23, 2020

MSOLLA AWEKEA MSISITIZO, USAJILI HUU YANGA NI BALAA TUPU

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla ameliambia chanzo chetu kwamba usajili wa Yanga msimu huu ni wa mafanikio makubwa.

Msola ambaye kitaaluma ni kocha alisema katika wachezaji wao watano wa kigeni hakuna mtu mwenye mashaka na vifaa hivyo kwani pesa zilizotumiwa na wadhamini wao GSM zimetumika kihalali.

“Usajili huu ni mkubwa na kiukweli tangu niingie ndani ya uongozi safari hii naweza kusema tuna kikosi ambacho kitarudisha heshima yetu,”alisema Msola.

Akiwageukiwa wachezaji wazawa waliosajiliwa Msolla alisema nao wamethibitisha ubora wao ambapo kwa ambao hawakupata nafasi ya kuanza wanatakiwa kutambua hiyo ni hatua ya upana wa kikosi na kwamba wana nafasi ya kuzidisha mapambano ya kuwania nafasi katika kikosi cha kwanza.

“Unajua hiyo ndio faida ya kuwa na upana wa kikosi yoyote ana nafasi ya kucheza muhimu ni juhudi zako kwenye mazoezi mpaka kwenye mechi siku ukipata nafasi.

“Ukiwachukua hawa wapya sasa ukawaunganisha na hawa waliowakuta utakuja kugundua kwamba msimu huu tuna timu bora sana,”aliongeza Msolla

1 thought on “MSOLLA AWEKEA MSISITIZO, USAJILI HUU YANGA NI BALAA TUPU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *