October 28, 2020

ZLATKO ATAKA MASHUTI MAKALI YANGA, TONOMBE AFUNGUKA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha mkuu Yanga Zlatko Krmpotic ni kwamba amekuwa akiwahimiza wachezaji wake kupiga mashuti makali wanapokaribia katika lango la wapinzani na sasa yanapigwa mengi.Faida kubwa ya ubora huo ndio ukazalisha bao bora la kiungo mkabaji Mukoko Tonombe akifunga kwa shuti kali bao la pili la timu hiyo katika ushindi wa juzi wa mabao 2-0 dhidi ya Mlandege ya Zanzibar.

Mbali na shuti hilo la Tonombe pia ubora huo ulionekana kwa mshambuliaji Yacouba Sogne, beki wa kulia Kibwana Shomari, Feisal Salum, winga Tuisila Kisinda na Carlinhos. Wamekuwa watu wa mashuti makali na ya mbali ambayo yamekuwa pia burudani kwa mashabiki.

Akizungumza na chanzo chetu, Kiungo Mukoko Tonombe alisema kocha wao anataka kuona viungo wanakuwa na akili ya kutengeneza mashambulizi ya haraka kwa pasi zao za kwenda mbele na zinazofika.

Tonombe alisema ukiwa na ubora wa kupiga pasi ndefu au hata fupi lakini za kwenda mbele ni rahisi kuishi na kocha huyo huku pia akiwataka kujaribu kwa kupiga mashuti makali kila wanapokaribia katika uso wa goli.

“Unaona kila wakati tunaangalia mbele anataka kuona tunapiga pasi zinazofika ukiweza kupiga ndefu zaidi ni hatua nzuri lakini iwe na uhakika,”alisema Tonombe.

“Anataka pia tupige mashuti pale tunapopata nafasi ya kupiga nafikiri ni kocha mzuri anayelenga kutaka matokeo nafurahi kufanya naye kazi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *