October 23, 2020

HIKI HAPA KIKOSI KAMILI YANGA KILICHOTINGA KAGERA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic amewaacha Dar es Salaam wachezaji wake saba katika kikosi kilichokwenda Bukoba jana kucheza na Kagera Sugar kesho Jumamosi.

Mastaa hao saba ambao waliachwa ni kipa Mkenya Farouk Shikhalo ambaye aliumia siku chache kabla ya kucheza mechi ya ligi na Mbeya City.

Wengine ni Abdulaziz Makame, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Juma Mahadhi, Paul Godfrey ‘Boxer’, Mapinduzi Balama ambaye bado ni majeruhi na Adam kihondo.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema Zlatko alitaka kusafiri na wachezaji 20 wanaocheza mechi moja na kurudi kabla ya kwenda Morogoro.

Wachezaji 20, waliosafiri ni Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili, Kibwana Shomary, Yassin Mustapha, Adeyun Saleh, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Said Juma, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Haruna Niyonzima, Tuisila Kisinda, Michael Sarpong na Yacouba Sogne. Carlinhos, Ditram Nchimbi, Deus Kaseke, Waziri Junior, Zawadi Mauya na Farid Mussa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *