October 28, 2020

MICHAKATO INAENDELEA, UJENZI UWANJA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ya klabu Injinia Bahati Mwaseba ameiambia chanzo chetu kuwa hatua ya awali ya kutafuta michoro ya ujenzi wanaoutaka katika eneo la Kigamboni imekamilika.

Mwaseba alisema baada ya kupata michoro sasa itakabidhiwa kwa Kamati ya Utendaji chini ya Mwenyekiti wao Dk Mshindo Msolla ambako huko watabariki au kuamua vinginevyo.

“Michoro tumeshaipata hiyo ni hatua ya kwanza na hatua inayofuata sasa ni kuwasilisha michoro hiyo kwa Kamati ya Utendaji na baada ya hapo tutakwenda hatua ya pili ya kutangaza ile tenda ya mradi,” alisema Mwaseba na kuongeza;

“Huu mradi utafanyika kwa awamu tatu unajua pale kutakuwa na vitu vingi mbalimbali tofauti ambavyo vitatoa maana kubwa kwa kile ambacho klabu yetu itakuja kukipata, hivyo tumepambana kukamilisha michoro hiyo.”

Mwaseba alisema katika mradi huo sasa watatangaza ili kupata kampuni itakayokidhi viwango na kujua gharama halisi zitakazohitajika kukamilisha kila kitu.

“Picha halisi tuliyoikamilisha ni kwamba pale tutakuwa na hivyo viwanja viwili vya kuchezea mpira wa miguu kitakachokuwa ana nyasi za kawaida na bandia, uwanja wa kikapu, netiboli, hosteli za watoto na wakubwa lakini pia tutakuwa na bwawa la kuogelea,” alisema Mwaseba kuhusu mchakato huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *