October 31, 2020

JESHI YANGA LATUA BUKOBA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kikosi cha Yanga kimetua kwenye Uwanja wa ndege wa Bukoba mapema hii leo asubuhi tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Yanga imeondoka na kikosi chake kamili baada ya kucheza mchezo wake wa kirafiki siku ya Jana dhidi ya Mlandege Fc uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi nakufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mara baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Kagera kikosi hiko kinatarajia kwenda mkoani Morogoro kuvaana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *