October 25, 2020

NIYONZIMA AAHIDI MAKUBWA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema usajili uliofanywa na Yanga, msimu huu umeongeza presha kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Niyonzima akizungumza na chanzo chetu, alisema ana matumaini makubwa ya mafanikio kwa namna kila mchezaji anavyojituma.

“Ukweli tupo kwenye presha kubwa hivi sasa, wachezaji pamoja na benchi la ufundi, unajua viongozi  na hata mashabiki wetu wanachotaka ni ushindi na ubingwa, hiyo imeongeza ushindani hata sisi wenyewe kwa wenyewe mazoezini,” alisema Niyonzima.

Kiungo huyo alisema hivi sasa kila mchezaji kambini amekuwa akipambana kuhakikisha anakuwepo kwenye kikosi cha kwanza.

Niyonzima ameeleza  kua  kwa ari waliyokuwa nayo hivi sasa kambini anaamini msimu huu mambo yatakuwa mazuri na mashabiki wao wajiandae kibeba kombe mwishoni  mwa msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *