October 31, 2020

MUKOKO TONOMBE APELEKA KILIO MLANDEGE

Msomaji wa Yanganews Blog:Klabu ya Yanga SC leo imecheza mchezo wake wa kirafiki kuelekea mechi yake ya Ligi Kuu Tanzania bara itakayochezwa wikendi hii Bukoba dhidi ya Kagera Sugar.

Kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu leo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa ligi kuu visiwani Zanzibar,Mlandege FC katika uwanja wa Chamazi jijini Dar Es Salaam na kupata ushindi wa magoli 2-0.

Yanga wametumia vikosi viwili tofauti kwa vipindi viwili walicheza mpira wa kuumiliki na kuanzisha mashambulizi kutokea pembeni.

Yanga imeshinda mabao 2-0, la kwanza limewekwa wavuni na Waziri Junior kwa mkwaju wa penalti dakika ya 40 na la pili limefungwa na Mukoko Tonombe aliyepiga shuti kali nje ya boksi lililoenda kwenye wavu na kumshinda kipa wa Mlandege dakika ya 59 baasa ya klutengewa mpira na Sogne.

Kikosi kilichoanza Yanga kabla ya mabadiliko golini alikuwa Metacha Mnata, mabeki Kibwana Shomari, Adeyun Salehe, Said Makapu, Abdallah Ninja, viungo Fei toto, Abdulaziz Makame, Farid Mussa, Haruna Niyonzima, washambuliaji Ditram Nchimbi na Waziri Junior.

Mlandege walicheza kwa kujiamini na kushambulia kwa kushtukiza japo mashambulizi yao hayakuwa na madhara kwa lango pinzani. Kipindi cha pili Mlandege walipata kadi nyekundu baada ya Ibrahim Juma kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Wachezaji walioingia kipindi cha pili walibadilisha mchezo wakiongozwa na Deus Kaseke, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong, Carlos Carlinhos na Zawadi Mauya huku langoni akiingia Ramdhan Kabwili.

Raundi ya tatu ya Ligi Kuu Bata itaendelea wikiendi hii ambapo Yanga itasafiri kwenda Bukoba kukipiga na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *