October 31, 2020

KOCHA WA VIUNGO YANGA APEWA RUHUSA , BUMBULI ATHIBITISHA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kukosekana kwa makocha wawili raia wa afrika Kusini , mechi dhidi ya Mbeya City, kumeibua sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii, uongozi umefafanua wameondoka nchini lakini kwa ruhusa maalumu.

Makocha hao ni Reidoh Berdien ambaye ni kocha msaidizi wa tatu akiwa na utaalamu wa mazoezi ya viungo, pia daktari wa viungo, Farid Caseem.

Katika mechi dhidi ya Mbeya City hawakuonekana kwenye benchi badala yake alikuwepo Kocha Mkuu Zlatko Krmpotic na msaidizi wake wa kuwanoa makipa Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi.

Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema wawili hao wamerudi kwao Afrika Kusini kwa mapumziko ya muda mfupi kwa kuwa makocha hao hawakupata muda wa kupumzika ligi ilipomalizika hasa baada ya Luc Eymael kupigwa chini.

Amesema wawili hao watarejea nchini baada ya wiki moja kuja kuendelea na majukumu yao.

Bardien na Caseem walikuja nchini kwa kuletwa na aliyekuwa kocha wa Yanga Luc Eymael ambaye baadaye alitimuliwa lakini Yanga alithibitisha wawili hao wataendelea kubaki katika ajira zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *