October 20, 2020

ALICHOSEMA MENEJA YANGA KUELEKEA MECHI YA LIGI KUU DHIDI KAGERA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Kuelekea mechi ya ligi kuu dhidi Kagera Sugar, meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema katika kukijenga vema kikosi kuelekea mchezo huo wa kwanza wa ugenini, leo usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini, Dar es Salaam, walitarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege kutoka Zanzibar.

“Tutacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege, hii itampa mwanga wa kuona maelekezo yake aliyowapa wachezaji mazoezini walivyoyafanyia kazi, itamsaidia kiufundi kubaini mahali walipoimarika na idara inayohitaji kuboreshwa,” alisema meneja huyo.

Alisema wanatarajia kuondoka jijini kesho na kuelekea Bukoba huku wachezaji wao wakiwa ‘fiti’ kwenda kupambana kusaka ushindi dhidi ya Kagera Sugar ambayo pia imekuwa ikiwasumbua kila wanapokutana.

Yanga inakutana na Kagera Sugar ambao wametoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina FC kwenye Uwanja wa Gwambina Complex wakati wao wanakumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *