October 20, 2020

ZLATKO AAHIDI FURAHA YANGA KUELEKEA MECHI YA LIGI KUU DHIDI KAGERA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Akizungumza na chanzo chetu hapo jana Zlatko alisema kikosi chake kipo tayari kwenda kupambana katika mchezo huo na mingine ya ugenini kwa sababu wanahitaji kupata pointi tatu kwenye kila mechi.

Zlatko alisema licha ya kupata ushindi katika mechi iliyopita, anayafanyia kazi mapungufu ya kikosi chake na anaimani ya kufanya vizuri katika michezo yao ijayo ikiwamo dhidi ya Kagera Sugar.

Kocha huyo alisema anahitaji timu yake kucheza soka la kiwango cha juu na ili kufikia huko, kila mchezaji anatakiwa kuonyesha uwezo wake halisi baada ya kukamilisha programu maalumu za mazoezi alizotoa.

Alisema kwa muda mfupi alikuwa nao amebaini wachezaji wake wanahitaji mazoezi kujijenga ambayo yatawaimarisha na kuwasaidia kuingia kwa haraka katika mfumo wake ambao utawafanya wapate matokeo mazuri katika mechi zinazofuata.

“Bado timu haijacheza vile ninavyotaka, ila wachezaji wangu wanapambana na kujitoa, nina imani kila siku zinavyozidi kwenda, kikosi kitakuwa imara, sasa akili yetu inajiandaa na mechi ijayo, tutahakikisha pia tunapata alama zote tatu muhimu katika mchezo huo,” alisema Zlatko

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *