October 31, 2020

KOCHA MKUU YANGA ATHIBITISHA, CARLINHOS BADO HAJAWA ‘FITI’

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha mkuu Yanga, Zlatko Karmpotic, amesema Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ni mchezaji mzuri, lakini kwa sasa hajawa tayari kuonesha makali yake.

Carlinhos ndiye aliyepiga kona iliyounganishwa kwa kichwa na Lamine Moro dakika ya 87 na kwenda moja kwa moja nyavuni na kuifanya Yanga kuzoa pointi tatu muhimu kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam juzi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Karmpotic alisema licha ya mchezaji huyo kuonesha ubora wa kutumia vema mipira iliyokufa kwenye mechi hiyo, lakini hawajawa tayari kuingia kwenye mfumo, hivyo bado anamuandaa ili arejee kwenye makali yake.

“Carlinhos ni mchezaji mzuri bado namuaandaa sitaki kumuua, ila amekuwa akilazimika kutokea benchi, namuaandaa ili afiti kwenye kikosi kwani ana muda mrefu hajacheza mpira kwao Angola ambako alikaa kwa zaidi ya miezi mitano kwa sababu ya corona,” alisema Karmpotic.

Pia aliwagusia wachezaji wengine akiwemo Yacouba Sogne, akisema naye hajawa kwenye kiwango chake, kwani amekaa bila kucheza mpira kwa miezi minne, hivyo sio kazi rahisi kwa kocha kukitengeneza kikosi kwa mara moja anatakiwa kupewa muda wa kutosha kutengeneza muunganiko.

“Michael Sarpong kwenye mchezo wa leo (juzi) hajafunga, ni mchezaji mzuri, ameonesha mchango mkubwa kwa kutengeneza nafasi na kuwasumbua wapinzani wetu,” alisema.

1 thought on “KOCHA MKUU YANGA ATHIBITISHA, CARLINHOS BADO HAJAWA ‘FITI’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *