October 25, 2020

BAADA YA KUITUNDIKA MBEYA CITY, SASA NI ZAMU YA KAGERA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Yanga SC jana imepata ushindi wake wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2020/21 katika uwanja wa Mkapa kwenye game waliyocheza na Mbeya City.

Kikosi cha Yanga ambacho kina muunganiko wa Wachezaji wapya wengi, kimefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 ikiwa ni goli pekee lililofungwa na Lamine Moro dakika ya 86.

Ushindi huo unaifanya Yanga SC kuwa na point 4 .

Sasa Yanga anaanza safari ya kwenda Bukoba kucheza dhidi ya Kagera Sugar September 19 na baadae kurejea Morogoro September 27 2020 kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *