October 28, 2020

HUKO YANGA HAKUNA KULALA AISEE

Msomaji wa Yanganews Blog:Huko Yanga haitaki kupoa baada ya kutoka kuvuna pointi tatu dhidi ya Mbeya City, kesho Jumatano inajipima ubavu na Mlandege ya Zanzibar, mchezo utakaopigwa saa 1:00 jioni.

Imeelezwa kwamba kocha wa timu hiyo, Zlatko Krmpotic anahitaji wachezaji wapate mechi nyingi zitakazowasaidia kuzoeana, ndio maana ameona siku siku tatu ambazo wanapumzika kusubiria mechi na Kagera Sugar, ijipime na Mlandege, Uwanja wa Chamazi Complex.

“Mechi hiyo inachezwa kwa mambo mawili, wachezaji kupata muda wa kuzoeana, pia uwanja wa Kagera Sugar unatumia nyasi bandia, ndio maana akataka wazoee kwa kucheza Uwanja wa Azam Complex,” amesema mmoja wa kiongozi Yanga

Ameongeza kuwa “Kocha amesema anahitaji timu iwe na mechi nyingi, ili apate kombinesheni ya wachezaji itakayokuwa tishio kwa timu pinzani, kwani anaamini kikosi chake ni kizuri,”amesem

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *