October 23, 2020

NAHODHA YANGA KUTANGAZWA HIVI KARIBUNI

Msomaji wa Yanganews Blog:Katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara msimu huu, Yanga imeanza na manahodha wawili tofauti.

Katika mchezo wa kwanza dhidi Prisons Yanga ilimpa kitambaa Deus Kaseke, ambaye pia alikuwa kiongozi katika mchezo wa Wiki ya Mwananchi.

Juzi, Yanga ilipocheza dhidi ya Mbeya City mambo yakageuka na Haruna Niyonzima akavaa kitambaa cha nahodha huku Kaseke akianza kwenye mchezo huo.

Baadaye Niyonzima alipotoka kipindi cha pili kitambaa kikatua kwa beki aliyeipa Yanga ushindi Lamine Moro.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amelieleza chanzo chetu kuwa bado cheo hicho kilichoachwa wazi na aliyekuwa kiungo wao Papy Tshishimbi hakijapata mwenyewe rasmi.

Saleh, ambaye ni meneja mkongwe zaidi alisema kocha wa timu hiyo Zlatko Krmpotic hajafanya uamuzi wa nani awe nahodha wake.

“Kocha bado hajafanya uamuzi kwa sasa tunawapa nafasi kulingana na uzoefu kwa wale ambao, wanaanza uwanjani,” alisema na kuongeza:

“Kocha alitaka muda kwanza kuangalia nani atamfaa katika majukumu hayo, lakini siku si nyingi atafanya uamuzi wa kina nani watafaa katika majukumu ya kuwaongoza wengine uwanjani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *