October 28, 2020

MAUZO JEZI YANGA USIPIME, MZIGO MWINGINE KUSHUSHWA

Msomaji wa Yanganews Blog:Ijumaa ya wiki iliyopita Yanga ilitambulisha jezi za msimu huu mpya 2020/21 na jana wakatangaza kwamba, mzigo wote umekata fasta tu.

Jezi hizo ziliuzwa kila jezi moja Sh 35,000 ukiwa ni mzigo wa awali ambazo zote zimeshambuliwa kama njugu kwa mujibu wa Mkurugenzi wa GSM, Hersi Said ambao ndio wasambazaji na wauzaji rasmi wa uzi huo.

“Tulileta jezi 8,000 tu na hizo zilikuja kwa ndege na leo (jana) zinakuja nyingine 8,000 tunawashukuru wanayanga kwa kununua bidhaa zao ila wasijali mzigo utakuja mwingi sana,” alidai Hersi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga.

Alidai mzigo huo wa awali umeuzwa jijini Dar es Salaam pekee huku utakaoingia ndio utasambazwa katika maeneo mengine nchini.

Aliongeza kuwa walichelewa kutambulisha jezi hizo na kuzileta hapa nchini kutokana na changamoto ya corona.

“Tutakuwa nazo jezi zenye majina ya wachezaji wetu, tutazitengeneza kwa oda maalum kwa watu wetu mfano jezi ya Tonombe mtu anaweza kuhitaji idadi fulani tukamte ngenezea,” alisema Hersi.

Alisisitiza kuwa kwa sasa wameanza na jezi huko usoni watakuwa na vifaa mbalimbali vyenye nembo ya klabu hiyo ambazo wanayanga watapata fulsa ya kuziotumia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *