October 25, 2020

YANGA KUKINUKISHA KESHO, MECHI YA KIRAFIKI DHIDI MLANDEGE

Msomaji wa Yanganews Blog:Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Yanga kesho itacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi mabingwa wa Ligi Kuu visiwani Zanzibar, Mlandege katika kujiweka sawa kuwakabili Kagera Sugar kwenye mchezo ujao.

Yanga itacheza mchezo huo majira ya Saa 1 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamanzi kabla ya kusafiri kwenda mkoani Kagera kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa siku ya Jumamosi 18 septemba, 2020 kwenye dimba la Kaitaba.

Mchezo huo ambao utakuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga ili kujiweka sawa kwa kuwa imefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake ambacho kina wachezaji wapya zaidi ya 12.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo, huku ikiwa imeshacheza michezo miwili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na kuambulia alama 4, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na kutoka sare na Tanzania Prisons.

Mlandege FC wao watatumia mchezo huo kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *