October 31, 2020

SENZO ALIANZISHA,MCHAKATO WA MABADILIKO YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Uongozi wa Yanga umesema Senzo Mazingisa ameanza majukumu yake Yanga, kwa kufanya mambo matatu, kutengeneza mfumo wa uendeshaji, kusimamia kamati ya katiba na ile ya mabadiliko.

“Majukumu yake kwa sasa ni kuishauri klabu katika mchakato ambao tunaufanya na watu wa La Liga,” alisema Makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela.

Alisema tayari ameshiriki vikao vingi katika kushauri kuelekea kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

“Vingi vimefanyika tangu ameingia Yanga, lakini makubwa ni lile la kutengeneza mfumo wa uendeshaji, kusimamia kamati ya katiba na ya mabadiliko,” alisema Mwakalebela.

Awali, Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla alisema wapo kwenye mchakato wa kukamilisha andiko la kwanza la muundo mpya wa klabu hiyo.

“Kamati ya Sheria na Katiba italipitia kisha viongozi wa matawi nchi nzima watapelekewa na kutakuwa na kablasha la katiba pendekezo na muundo pendekezo.

“Tutatoa wiki tatu za majadiliano na kuvipitia kabla ya kwenda kwenye mkutano mkuu, ambao ajenda zitakuwa mbili, mabadiliko ya katiba na muundo wa uendeshaji wa klabu.

“Tukikamilisha mchakato wa mabadiliko, tunaachana na mambo ya katibu mkuu na mwenyekiti, tunaingia kwenye mfumo mpya,” alisema Dk Msolla

Kwa habari zaidi Download app ya Yanganews toleo jipya kutoka playstore. Bonyeza picha hapa chini

1 thought on “SENZO ALIANZISHA,MCHAKATO WA MABADILIKO YANGA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *