October 23, 2020

JEZI ZA MABINGWA KUZINDULIWA LEO

Msomaji wa Yanganews Blog:Hatimaye Yanga imethibitisha kwamba itazindua jezi zao za msimu mpya leo Septemba 10, 2020 makao makuu ya klabu yao Mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Mhandisi Hersi Said amesema uzinduzi huo utafanyika leo makao makuu ya klabu hiyo kuanzia majira ya saa 4:30 asubihi katika duka maalum walilolitengeneza.

Hersi ambaye kampuni yao ndio yenye jukumu la kuzalisha na kusimamia mauzo ya jezi na vifaa vingine amesema mara baada ya uzinduzi huo haraka jezi hizo zitaanza kuuzwa hapohapo kwa mashabiki wao.

“Tulitaka kuanza kuuza jezi zetu zikiwa zimefika kwa idadi ya kutosha kuweza kutosheleza soko la wadau wetu ambao kiukweli walikuwa na kiu kubwa ya kuona na kununua jezi zao za msimu huu na uzinduzi rasmi utafanyika kesho,”amesema Hersi.

Hersi ameongeza kuwa katika hatua ya awali ya kuuzwa kwa jezi hizo zitakazopatikana sokoni ni zile za daraja la kwanza ambazo zitauzwa kwa sh 35,000.

“Tukishafanya uzinduzi mbali na kuuzwa pale katika duka letu maalum makao makuu pia zitapatikana katika maduka yetu yote ya GSM na sehemu zingine ambazo tutawatangazia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *