October 28, 2020

ALICHOSEMA MAKAMU MWENYEKITI YANGA KATIKA UZINDUZI JEZI MPYA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Klabu ya Yanga imetambulisha rasmi  jezi mpya   watakazotumia msimu huu wa Ligi Kuu Bara katika  michezo  ya nyumbani na ugenini.

Makamu Mwenyekiti , Frederick Mwakalebela amesema kilichochangia kuchelewa kwa jezi zao mpya ni janga la virusi vya corona.

“Kwanza nianze kwa kuomba radhi kwa mashabiki na wanachama wa Yanga. Janga la virusi vya corona limeathiri mambo mengi ikiwemo hili ndio maana  jezi zimechelewa kufika,” amesema Mwakalebela.

Akizungumzia jezi hizo katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Injinia Hersi Said amesema klabu yao ni ya wananchi hivyo muundo wa jezi umeendana na hilo.

“Jezi zimeendana na Utanzania na zinaonyesha kuwa sisi ni Waafrika. Leo (Ijumaa) tumezindua jezi mbili ambazo ni za nyumbani na ugenini lakini baadaye tutazindua jezi ya tatu,” amesema.

Hersi ameongeza kwa kusema kila mwaka watakuwa wakitengeneza jezi ambazo zitakuwa na mlengo maalum.

 

Upande wa mshauri wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa Mbatha amesema ni vema mashabiki kuchangia mapato ya klabu yao kwa nunua jezi hizo.

“Kununua jezi ni sehemu ya mfumo mpya tunaoundea . Nitoe wito kwa mashabiki wa Yanga kuisapoti klabu yao kwa kununua jezi orijino,” amesema Senzo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *