October 25, 2020

ALICHOSEMA KOCHA MKUU YANGA KUELEKEA MECHI YA LIGI KUU DHIDI MBEYA CITY

Msomaji wa Yanganews Blog:Kuelekea mechi ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City,Kocha Mkuu wa Yanga amesema kwa sasa anaendelea kuyafanyia kazi mapungufu aliyoyaona katika mechi ya kwanza kwa lengo la kuhakikisha wanaibuka na ushindi Jumapili.

Kocha huyo alisema timu yake bado ni mpya na anahitaji muda mfupi wa kutengeneza muunganiko mzuri ambao utamsaidia kufanikisha ushindi na anaamini mechi inayofuata wataingia wakiwa imara zaidi.

“Timu haikuwa na muda mrefu wa maandalizi, tunatumia muda huu uliopo kujiandaa na kujenga kikosi imara, pia kujenga muunganiko wa wachezaji, tutakuja kufanya vizuri mbele katika mechi zetu zijazo,” alisema Zlatko.

Alieleza timu yake haikuwa na katika kiwango bora katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons, lakini walishindwa kutumia vema nafasi zote walizopata.

“Baada ya kuona wachezaji hawako ‘fiti’ na tatizo la pumzi ambalo linawafanya wanashindwa kumudu kucheza dakika 90, nimeshaanza kutatua tatizo hili, pia wanatakiwa kuongeza utulivu na umakini,” Zlatko alisema.

Alisema wana nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zinazofuata kutokana na kupata muda zaidi wa kuwanoa tofauti na alivyoikuta timu, siku chache kabla ya msimu mpya haujaanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *