October 23, 2020

TONOMBE AWATOA HOFU WANAYANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kiungo mpya wa Yanga Mukoko Tonombe amewataka mashabiki hao wa Jangwani watulie, kwani kama ni ishu ya ubingwa kwa Yanga msimu huu ni jambo lisilokwepeka kwa aina ya kikosi walichonacho na alichokiona ndani ya wiki mbili tangu ajiunge na timu hiyo.

Kiungo huyo kutoka DR Congo, ameliambia chanzo chetu baada ya kukaa na wenzake kwa wiki mbili amegendua muunganiko wao kama utakubali haraka basi ushindi utakuwa mkubwa katika mechi zao na haoni kitu kitakachowazuia wasiubebe ubingwa msimu huu.

“Watu wana wasiwasi na sare? Hapana waambieni watulie mbona hii timu ni bora! Tutakuja kushinda tena vizuri tu, nimeona tuna timu nzuri wala hakuna wasiwasi ni suala la muda tu,” alisema Mukoko aliyesajiliwa na Yanga akitokea AS Vita ya DR Congo na kuongeza:

“Timu inajengwa, ingekuwa mbaya kuanza ligi kwa kufungwa, lakini tulipata sare, binafsi naona ilicheza vizuri sana magoli yalikataa tu kuingia ile mechi lakini yatafungwa mengi tu.”

Kiungo huyo mkabaji alisema ubora tofauti wa wachezaji wapya na wenzao waliowakuta unampa imani watakuwa katika afya nzuri ya kuchukua mataji msimu huu.

Alisema hatua nzuri katika kikosi chao wamekuwa wakihimizana juu ya kuhakikisha wanashinda katika mechi zao na kwamba makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa kwanza yatarekebishwa katika mchezo ujao.

“Uzuri katika timu naona wapo wachezaji wenye uzoefu mkubwa, wale ambao wanaonekana kupungua uzoefu nao watajifunza ndio maana ya timu ila tuna timu nzuri ya kuchukua ubingwa. “Kila mchezaji hapa anataka kuona tunashirikiana na tunashinda, hiyo ni hatua kubwa ukiwa katika kikosi cha namna hiyo, hatukushinda mchezo uliopita lakini kuanzia mechi ijayo watu wataona,” alisema kiungo huyo. Katika mechi na Prisons, Mukoko na Tuisila walianzia benchi kabla ya kuingia kipindi cha pili na kuichangamsha timu, huku ikipoteza nafasi nyingi za wazi.

Mukoko alisema licha ya kwamba yeye ni mgeni nchini, lakini ameiangalia ligi kwa mechi za awali na kubaini itakuwa na ushindani kwanui kuna timu zinaoonekana kuwa bora, lakini ubora wao haushindani na Yanga chini ya kocha wao, Zlatko Krmpotic ambaye ameungana nao hivi karibuni kutoka Serbia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *