October 28, 2020

RASMI:JEZI MPYA YANGA YAZINDULIWA

Msomaji wa Yanganews Blog:Uzinduzi umefanyika Makao Makuu ya Klabu Jangwani Dar es Salaam, ambao zimezinduliwa jezi za nyumbani, ugenini pamoja na za golikipa.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambayo ndio mzalishaji na msambazaji wa Jezi za Yanga, Eng Hersi Said amesema jezi hizo mpya ni za kisasa na zimezingatia vigezo vyote vya ubora.

“Jezi hizi zinaubora wa hali ya juu, tumezingatia ubora ili Wananchi wapate kitu kilichobora,” amesema.

Jezi zilizozinduliwa ni za nyumbani ambazo ni za rangi ya kijani na bukta nyeusi wakati za ugenini ni Njano na bukta nyeusi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa viongozi mbalimbali wa Yanga wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *