October 20, 2020

CARLINHOS KUTUMIWA MARA CHACHE, KUKINUKISHA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic amesema Carlos Fernandez ‘Carlinhos’ bado hayupo fiti kukipiga dakika 90, badala yake atakuwa akimtumia muda mchache.

Krmpotic alisema Carlinhos ni mchezaji mzuri mwenye kipaji lakini si muda wake wa kucheza mechi dakika zote haswa katika mechi za aina ya Tanzania Prisons.

“Wapinzani walikuwa wazuri kwenye nguvu kama timu na hata mchezaji mmoja mmoja, Carlinhos maandalizi yake hayakuwa ya kutosha kucheza mechi ya aina ile (Prisons) yenye matumizi makubwa ya nguvu kwani ilitaka mchezaji aliye fiti zaidi,” alisema.

“Nitaendelea kumuandaa Carlinhos aweze kuwa fiti na kutumika zaidi katika michezo ijayo atakapokuwa tayari kwani ni mchezaji mwenye kipaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *