October 28, 2020

KUBWA KULIKO KUJENGA UWANJA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Yanga imewashukuru mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga waliojitokeza kwa wingi katika kilele cha Wiki ya Mwananchi huku wakisema wana madeni matatu makubwa kwao.

Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz amesema licha ya kufanya vizuri katika kilele cha Wiki ya Mwananchi wana madeni matatu kwa mashabiki wao.

Nugaz amesema deni la kwanza ni uzinduzi wa duka la klabu hiyo ambalo ujenzi wake unaendelea kwenye makao makuu ya Yanga Jangwani.

“Tutafanya uzinduzi wa duka letu hivi karibuni na tutakuwa klabu ya kwanza kuzindua duka lake makao makuu ya klabu”

Yanga imesema deni la pili ni suala la jezi ambalo limekuwa linapigiwa kelele na mashabiki wao waliokuwa na shauku ya kuona uzi mpya wa msimu huu 2020/21.

“Pia tuna deni la kuingiza mzigo mpya wa jezi mpya  na zitakapofika wanachama na mashabiki wataambiwa kwani tunataka kila shabiki avae jezi halisi ya timu”

Nugaz alisema deni la tatu ni upatikanaji wa uwanja wa kisasa utakaotumiwa na wanajangwani hivyo wataandaa tukio la kubwa kuliko ili kuanza uchangjaji wa uejnzi.

“Lakini pia tunajiandaa na tukio la kubwa kuliko ambalo lengo la tukio hilo litakuwa tofauti na lile tulilolifanya safari hii litakuwa kwa ajili ya kuanza safari ya ujenzi wa uwanja wetu wa Kigamboni”, amesema Nugaz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *