October 28, 2020

UONGOZI WAPELEKA SHUKRANI KWA MASHABIKI YANGA ‘WIKI YA MWANANCHI’

Msomaji wa Yanganews Blog:Uongozi wa Yanga ukizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi, umepeleka shukrani kwa mashabiki wa Yanga ‘wiki ya mwananchi’

Nukuu, akizungumza mwenyekiti Kamati ya Hamasa katika mkutano na waandishi wa habari hii leo.

Mosi, nichukue fursa hii kuwashukuru wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa kushiriki kikamilifu shughuli zote za Sportpesa Wiki ya Mwananchi 2020 tangu zilipozinduliwa rasmi tarehe 22/08/2020 kule Dodoma. Kujitoa kwenu kwa wahitaji, kuchangia damu, kufanya usafi na kurejesha kwa jamii ndio dhima kuu ya sherehe hizi za wiki ya mwanachi kwa klabu yetu.

Pili, nawashukuru wachama wetu wote, wapenzi na mashabiki nchi nzima kwa kujitokeza kwa maelfu kuja uwanjani na kuujaza uwanja wa Mkapa siku ile ya kilele cha Sportpesa Wiki ya Mwanachi 2020 tarehe 30/08/2020 pale Uwanja wa Mkapa; Na kushuhudia kile ambao tuliandaa kwa ajili yenu; ambazo ni burudani kutoka kwa wasanii wetu pendwa ambao pia ni wananchi, na kikubwa zaidi ni burudani ya soka kwa timu zetu zote za wanawake, na vijana, kadhalika kamati ya utendaji, sekretarietina Kamati zetu zingine.

Kipekee kabisa nawashukuru wanachama wetu, wapenzi namashabiki waliosafiri kutoka mikoani kuhudhuria kilele cha wiki ya mwanchi, ahsanteni sana.

Kadhalika, tunatoa shukrani kwa wadhamini wetu wote, Sportpesa, GSM, Taifa Gas, Afya Water, na Azam Media kwa udhamini wao ambao ndio mafanikio ya Wiki yetu hii.

Tunaamini ushrikiano huu utaendela ili kujenga mchezo wa soka na kuikuza dhana ya Soka la Matumani ‘Football of Hope’ kwa kurejesha kwa jamii kila mwaka katika msimu wa wiki ya mwanachi.

Nichukue fursa hii kuwakaribisha wadau wengine na wapenda michezo kujiunga nasi katika kuikuza dhana hii ya soka la matumaini kua sehemu ya kujenga uchumi, kuibua vipaji na ajira na kuineemesha jamii kwa matumaini na kuipa bega la kujishikiza; kubwa kaliko yote ni kuleta
burudani na ushindani katika kukuza soka letu.

Mwisho katika shukrani, lakini sio kwa umuhimu, nawashukuru wasanii wetu wote waliopamba
shughuli yetu hii, wale wa bongo fleva, singeli na kadhalika. Pia Vyombo vyoye vya habari ambayo mmekua nasi bega kwa bega kuwahabarisha wanachama, wapenzi na mashabiki matukio na taarifa za wiki yetu hii kwa mwaka huu. Tunaomba tuendelea kufanya kazi pamoja ili
tuwahabarishe watanzania wote juu ya habari zetu wanaYanga na soka letu kwa ujumla, ahsanteni sana.

Nichukue fursa hii pia kuwoamba radhi wanachama wetu, wapenzi na mashabiki ambao kwa mamia na maelfu walisalia nje na kushindwa kuingia ndani baada ya uwanja kujaa; mtusamehe sana. Niwaahidi kua wakati mwingine tutajiandaa kwa viwanja vyote viwili sababu mmeuthibitishia umma wa watanzania kua Yanga ndio mwamba wa soka Tanzania na anaengoza kwa wanachama na mashabiki wengi, na zaidi wale wahudhuriaji wa kuujaza uwanja.

Kwa niaba ya kamati naomba radhi kwa mapungufu yote yaliyojitokeza siku ya kilele na wakati wote wa sherehe za Sportpesa Wiki ya Mwanchi 2020. Ninaomba kuyabeba yote. Lakini pale ambapo tumefanya vema, basi sifa ni kwetu sote sisi wanachi, maana shughuli ilikua yetu na
tumeitendea haki, na tunastahili kuendelea kuitwa Home of Champions na ‘Wananchi’. Hongereni sana.

Mwisho niwatakie msimu mwema wa Ligi unaoenda kuanza, tuendelee kujitokeza kwa wingi uwajani katika mechi zetu zote kuipa sapoti timu yetu na kushangilia kwa nguvu mwanzo mwisho, sababu ndio raha ya kua mwananchi.

Ahsanteni sana
Qs. Suma Mwaitenda;
Mwenyekiti, Habari na Hamsa Yanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *