October 28, 2020

MSHAMBULIAJI MWINGINE KUSAJILIWA YANGA ‘USAJILI DIRISHA DOGO’

Msomaji wa Yanganews Blog:Uongozi wa Yanga umesema wameanza mikakati ya kusajili beki wa kati na mshambuliaji mwingine ili kuimarisha kikosi na kutwaa ubingwa wa ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Hayo yalisemwa jana/juzi na Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, baada ya mchezo wa Wiki ya Mwananchi kumalizika na kushinda mabao 2-0.

Msolla alisema wachezaji waliosajiliwa ni wazuri na wameonyesha uwezo mkubwa pamoja na kufanya mazoezi kwa muda mfupi.

“Tuna timu nzuri, hilo halina ubishi na naamini, wapinzani wamezibwa midomo, zoezi la usajili limefungwa na sasa tunaelekea kwenye ligi, tutashusha ‘mashine’ mbili zaidi wakati wa dirisha dogo la usajili, lengo ni kuwa na kikosi kipana,

Tumeiona timu na jinsi walivyocheza, Lamine (Moro) hajacheza kutokana na majeraha na kulazimika kucheza Mwamnyeto (Bakari) na Ninja (Abdalla Shaibu) na baadaye Makapu, (Juma), kuna ulazima wa kuongeza beki mwingine eneo hilo,” alisema Msolla.

Alisema nafasi ya ushambuliaji imeonyesha kuwa ni moto, lakini wanataka kuwa na ushindani zaidi na hivyo atashusha mshambuliaji mwingine mbali ya Yacouba Sogne, Waziri Junior na Michael Sarpong.

Alifafanua kuwa mipango hiyo imeshakamilika na kilichobaki ni kufyatua tu.

Alisema kuwa mikakati yao ni kushinda kila mechi na kutwaa ubingwa mapema sana.

“Kimsingi, wachezji wetu wameonyesha uwezo mkubwa, wameonyesha kuwa wapo tayari kwa mashindano pamoja na kuwa na muda mfupi wa maandalizi, Yanga tofauti na timu nyingine, imecheza na timu ngumu, iliyokuwa imejiandaa kwa muda mrefu,” aliongeza kiongozi huyo wa Yanga, ambaye kitaaluma ni kocha pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *