October 25, 2020

ALICHOSEMA TUISILA KISINDA BAADA MECHI WIKI YA MWANANCHI

Msomaji wa Yanganews Blog:Licha ya kuonyesha makali katika mchezo wake wa kwanza kwenye mchezo wa kirafiki wa kilele cha Wiki ya Wananchi, winga mpya wa Yanga, Tuisila Kisinda ‘TK Master’ amesema bado kuna mambo ‘makubwa’ yanakuja, hivyo mashabiki watulie.

Mbali na uwezo mzuri aliouonyesha, nyota huyo juzi alifunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Eagle Noir ya Burundi, akipokea pasi ya kiungo, Feisal Salum ‘Feitoto’.

Akizungumza na chanzo chetu muda mfupi baada ya mchezo huo, Kisinda alisema yeye na wachezaji wenzake wa kigeni wana deni la kuwalipa mashabiki wa Yanga kutokana na hamasa waliyoionyesha tangu walipotua nchini na juzi walipoujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Nimependa hali ilivyokuwa uwanjani, bado naamini kuna mengi ya kuifanyia klabu hii, nawashukuru sana mashabiki tangu siku ya kwanza nilipofika hapa nchini mpaka kwenye mchezo huu,” alisema TK Master.

Nyota huyo aliyesajiliwa kwa pamoja na Mukoko Tonombe alisema yupo tayari kwa ‘mikiki’ ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki.

Yanga inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuanza msimu mpya kwa kuikaribisha Tanzania Prisons ya Mbeya, mchezo utakaofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *