October 28, 2020

ALICHOSEMA SOGNE BAADA YA KUTUA NCHINI ‘KUJIUNGA NA YANGA’

Msomaji wa Yanganews Blog:Mshambuliaji mpya wa Yanga, Yacouba Sogne amesema anafurahi kujiunga na timu hiyo na anaamini atapambana kuhakikisha anafanya vizuri ili kufikia malengo yanayotarajiwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Sogne alisema hayo jana mchana baada ya kuwasili nchini akitokea kwao Burkinafaso na kusaini mkataba wa miaka miwili.

“Nimefurahi kuona mapokezi makubwa ya mashabiki, lakini kuja kuichezea timu ya Yanga na kuhakikisha tunafikia malengo yanayotarajiwa,” alisema Sogne.

Naye Mkurugezi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Hersi Saidi, alisema nyota huyo amewasili ili kuja kuitumikia Yanga na sababu za kuchelewa zilitokana na kuwa nje ya uwezo wao.

“Tayari mchezaji huyu ni mali yetu, yupo tayari kuitumikia timu yetu kwa muda wote atakapokuwa katika klabu yetu,” alisema Hersi.

Nyota huyo wa zamani wa Asante Kotoko alitua nchini jana saa 7: 20 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea Addis Ababa akiwa ni mchezaji huru.

Sogne anaungana na wachezaji wengine wa kigeni wapya ambao ni Carlinhos, Michael Sarpong, Tusila Kisinda na Tunombe Mukoko ambao juzi walikuwa ni sehemu ya utambulisho katika sherehe za Siku ya Wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *