October 28, 2020

TAARIFA KUTOKA YANGA

 

Msomaji wa Yanganews Blog:Uongozi wa Klabu ya Yanga, tunalaani vikali kitendo kisicho cha kiungwana kilichofanywa na baadhi ya mashabiki wa timu yetu kwa kumpiga na kumchania nguo shabiki aliyekuwa amevalia jezi ya watani wetu wa Jadi, Simba.

Taarifa ya Klabu iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu,Wakili, Simon Patrick imesema Yanga tunaamini katika uungwana kwenye mchezo wa soka, hivyo kama klabu haiungi mkono vitendo vya aina yoyote vinavyoashiria kuvunja amani na kuondoa uungwana michezoni.

“Uongozi wa Yanga unawasisitiza wanachama, wapenzi na mashabiki kwamba upinzani na utani wa jadi haimaanishi chuki, uhasama au vita na kuhatarisha amani na usalama wa watu,” imesema sehemu ya taarifa ya Kaimu Katibu Mkuu

Daima Mbele Nyuma Mwiko

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *