October 28, 2020

ALICHOSEMA FARID MUSSA BAADA WIKI YA MWANANCHI

Msomaji wa Yanganews Blog:Kiungo mpya wa Yanga, Farid Mussa amesema mechi ya jana Jumapili Agosti 30, 2020 aliyocheza dhidi ya Aigle Noir ya Burundi, imempa picha ya nini anapaswa kukifanya msimu unaoanza Septemba 6.

Amesema ameona jinsi ambavyo mashabiki wana matumaini makubwa na kikosi chao, hivyo inamuongezea umakini wa kujituma zaidi kuwapa kile wanachokitarajia kutoka kwake.

Yanga imemsajili Farid akitokea Tenerife B ambayo aliichezea miaka mitano tangu alipojiunga nao mwaka 2016, akitokea Azam FC, amesema licha ya kucheza timu hiyo kwa mara ya kwanza lakini hana ugeni na Ligi Kuu Bara.

“Nimeona mwitikio wa mashabiki ambao unatafsiri kubwa kwetu, kuona ni namna gani ambavyo wanakiamini kikosi chao kwamba kitawapa furaha msimu huu, kwangu nimechukulia kama changamoto ya kuongeza bidii zaidi,”amesema Farid na kuongeza kuwa.

“Mara nyingi sipendi kuzungumza hovyo kwa sababu kazi ya soka ni wazi, natamani watu wawe wanaona wenyewe nini nafanya, kikubwa ni ushirikiano wao mashabiki ili tufikie malengo kwa pamoja,”amesema.

Ametoa mtazamo wake juu ya ligi msimu huu kwamba itakuwa na ushindani wa hali ya juu, ambao utawafanya wajitume na kuhakikisha wanaipambania timu yao kufikia malengo waliojipangia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *