October 28, 2020

STRAIKA MPYA ATUA KWA KISHINDO YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Straika mpya Yacouba Songné amewasili nchini leo kujiunga nasi Mabingwa wa Kihistoria Tanzania.

Nyota huyo raia wa Burkina Faso ametua mchana huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere na kulakiwa na mashabiki waliiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Eng. Hersi Saidi.

Eng. Hersi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni GSM ambayo imefadhili usajili wa wachezaji wapya kwenye kikosi cha Timu ya Wananchi.

Yacouba anakamilisha idadi ya wachezaji wapya walisajiliwa msimu huu, ambapo wengine walipata nafasi ya kutambulishwa Jana kwenye kilele cha tamasha la Wiki ya Mwananchi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *