October 25, 2020

STRAIKA BURKINAFASO KUTUA LEO

Msomaji wa Yanganews Blog:Straika mpya wa Yanga aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu , Mghana Yacouba Sogne anatarajia kutua leo Jumatatu Agosti 31, 2020 saa 7 mchana.

Jana Jumapili Agosti 30, 2020 katika kilele cha Wiki ya Mwananchi kilichofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa kutambulisha kikosi chao jina la mchezaji huyo pia lilitajwa na kwamba anaingia leo kuungana na wenzake.

Awali mchezaji huyo alitakiwa kutua nchini Agosti 28, 2020 mchana ambapo kama kawaida mashabiki wa Yanga walijazana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakisubiri kumpokea mchezaji wao.

Hata hivyo, uongozi wa Yanga ulitoa taarifa ya ghafla kwamba Yacouba asingetua siku hiyo kutokana na mabadiliko ya ratiba ya ndege.

Katika usajili wa msimu huu, mashabiki wa Yanga wamekuwa wakienda kuwapokea nyota wao wa kigeni ambapo walifanya hivyo walipotua Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko na Carlos Carlinhos.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *