October 28, 2020

NIYONZIMA APONGEZA USAJILI DIRISHA KUBWA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima, ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa usajili mkubwa wa kikosi chao, ambao wameufanya kuelekea msimu ujao.

Akizungumza na chanzo chetu, Niyonzima alisema usajili uliofanywa msimu huu unarudisha matumaini ya kurudisha mafanikio ya timu hiyo, ambayo yamepotea kwa misimu mitatu iliyopita.

“Niupongeze uongozi wangu kazi, waliyoifanya kuimarisha kikosi siyo ndogo naamini ule unyonge ambao walikuwa nao mashabiki wetu msimu uliopita niwaahidi kwamba hautokuwepo tena,” alisema Niyonzima.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, alisema kwa kutumia uenyeji wake kuwapa ushirikiano mzuri wachezaji wote wageni, lengo likiwa ni kurudisha furaha kwa mashabiki wao, ambao wamemaliza misimu miwili bila taji lolote.

Niyonzima alisema anatambua vizuri uwezo wa kocha mpya  wa timu hiyo Zlatko Krmpotic, na anaamini ataisaidia timu hiyo katika harakati zao za kurudi kwenye mafanikio yao.

Kiungo huyo amewaomba mashabiki wa Yanga kuendelea kuwapa sapoti na kufika uwanjani kwa wingi, ili kuwapa ari wachezaji wazidi kujituma ili kuipa mafanikio timu yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *