October 28, 2020

BUMBULI AWAITA MASHABIKI DIMBA LA TAIFA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kweli wananchi wameamua, kwani mpaka sasa wamemaliza tiketi za Royal ambazo zilikuwa zikiuzwa kwa Sh 200,000.
Mashabiki wamehimizwa kuendelea kununua tiketi ili kwenda kushuhudia wachezaji wao wapya katika kilele cha Wiki ya Mwananchi kesho  Jumapili.
Yanga itashuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa kuikabili Aigle Noir ya Burudi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kuhitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi.
Klabu hiyo inatumia tamasha hilo kutambulisha wachezaji wake watakaoitumikia Yanga kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao na mashindano yote.
Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema tayari wamemaliza tiketi za Sh 200, 000 huku tiketi nyingine zikiendelea kuuzwa kwa kasi.
“Tunashukuru mashabiki wameendelea kuitikia wito wa kununua tiketi na kumaliza hizo za Royal.
“Sasa hivi zimebaki tiketi za Sh 30000 kwa VIP A, wakati VIP B na C ni Sh 20,000 na mzunguko Sh 5000 hivyo tunawaomba mashabiki waendelee kununua tiketi ili kesho tukajaze uwanja”, amesema Bumbuli.
Bumbuli ametaja maeneo zinapopatikana tiketi kuwa ni Mwenge Sheli, Ubungo Sheli, Uwanja wa Mkapa, Kibo Complex Tegeta, Buguruni Sheli, Dar Live Mbagala, Makao makuu ya Yanga na maduka yote ya GSM.
Wakati huo huo,  Bumbuli amesema wamempokea kocha Mserbia ambaye ametua leo Jumapili asubuhi na leo hii jioni atahudhuria mazoezi ya mwisho ya  kikosi hicho yatakayofanyika Uwanja wa Mkapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *