October 23, 2020

NAAM….MORRISON ATAMBULISHWA KIKOSI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kama noma na iwe noma! Hiki ndio kinachoweza kuonekana kwa sasa baada ya Yanga kumtangaza Bernard Morrison kuwa miongoni mwa wachezaji wake.

Katika utambulisho wa kikosi cha Yanga kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, ambapo ilianza kwa wachezaji waliopo uwanjani na benchi zima la ufundi kisha ukaingia kwa Yacouba Sogne ambaye atatua nchini kesho Jumatatu ya Agosti 31, 2020.

Baada ya kumaliza utambulisho ya Sogne, shughuli ikamalizia kwa kumtambulisha Morrison.

Mshereheshaji wa shughuli hiyo Maulid Kitenge sambamba na Zembwala alianza kwa kusema: “Bwana Zembwela…. Waswahili wana msemo wao wanasemaaaa…Mke ambaye hujampa talaka bado ni mkeo, hivyo mchezaji wetu wa 28 ni Bernard Morrison”

Kauli hiyo iliibua shangwe kwa mashabiki wa Wananchi waliofurika uwanjani hapo huku wengine wakionyesha staili yake ya kushangilia wakati alipowapiga Simba bao kali la friikiki.

Tayari Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla amesema washapeleka rufaa iliyompa ushindi Bernard Morrison kuwa mchezaji huru kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS) kwa ajili ya hatua zaidi.

Amesema Morrison bado ni mchezaji wao halali kwa kuwa mapungufu ya kimkataba hayaondoi uhalali wa mkataba uliopo hivyo, watatafuta haki kwenye vyombo vya juu vya soka.

Pia, amesema kama Simba wanahitaji huduma ya Morrison basi milango iko wazi kwenda kuwasilisha ofa mezani huku akifichua kwamba, thamani ya winga huyo wa Ghana ni Sh600 milioni.
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *