October 25, 2020

UCHAMBUZI KIKOSI CHA YANGA , MECHI DHIDI AIGLE NOIR

Msomaji wa Yanganews Blog:Hans Van Hans van der Pluijm kwa nyakati tofauti akiwa kocha wa Yanga SC , alikuwa muumini sana wa mfumo wa 4-4-2, 4-3-3 na kwa mechi ngumu akibadilika kwa 4-5-1. Hakuna asiyeyajua mafanikio ya Yanga na mdachi huyo .

Ernie Brandts akiwa kocha wa Yanga SC alijaribu kuicheza timu hiyo kongwe zaidi nchini kwa mfumo wa 4-3-3 na 3-5-2 lakini alirudi kwenye 4-4-2.

George Lwandamina alipata kusema.. “ bado nina hitaji kutumia 4-4-2 ili kuipa balansi timu katika idara zote tatu huku kila mchezaji akiwa na jukumu mama kwa variations na patterns za total football. “ Sote tunamfahamu Lwandamina kwa upole wa sura yake lakini mbinu na mfumo wake huyu uliipa jeuri Yanga ambayo ilikuwa na kikosi cha average players ambao pia walikumbwa na ukata.

Ni ukweli usiopingika , unapokuwa na wachezaji wazuri kila idara ukatumia vyema 4-4-2 kwa approach nzuri , ni dhahiri timu inaakuwa na balance nzuri kimbinu na kiufundi pia rahisi sana kuona mchango wa kila mchezaji uwanjani. Huu ndio mfumo pekee ambao hata mlinzi anaweza kuibuka man of the match kwakuwa kila mchezaji uwanjani anakuwa ni sehemu ya attacking patterns na defensive patterns respectively.

Zlatico kocha mkuu Yanga SC sanjari na msaidizi wake Juma Mwambusi , wameirudisha Yanga kwenye patterns za 4-4-2 ambazo huifanya kuzalisha mawinga wazuri , walinzi wa pembeni na washambuliaji ambao huwa moto wa kuotea mbali kutokana na mipira mizuri kutoka pembeni na kati.

Makocha hawa kwa muda mfupi sana wameweza kuijenga timu kuelewana vyema kuanzia nyuma hadi mbele hususani kwa kikosi cha kwanza ambacho kilikuwa chini ya utawala wa Tuisila Kisinda kama kiungo mchezeshaji wa pembeni wakati huo huo akiwa na majukumu ya kiufundi kama invisible attacking midfielder nyuma ya Ditram Nchimbi na Sarpong . Makocha wa Yanga waliamua kuibana Aigle Noir upande wa kulia huku huku wakifungua njia kushoto kupitia kwa Tuisila Kisinda ‘ TK Master ‘ . Shomari akiwa na majukumu ya kuwabana Aigle kushoto huku akihakikisha anapata juu kama wing back ili kuongeza pressure ya mashambulizi pia akifanya mbinu za kukabia juu kama ambavyo 4-4-2 na mbinu zake inayoruhusu.

Mfumo huo uliwapa goli mbili Yanga SC kutoka kwa Kisinda na Sarpong na wote wakifunga kimbinu haswa baada ya timu kufanya extension ya kiungo chote cha kati kutanuka ili Aigle wajae kati kama njia halafu wao watanuke pembeni kwa kasi , kumbuka uchawi mkubwa wa 4-4-2 ni matumizi ya mawinga na kiungo cha kati kuwa solid na compact kuminya na kutanua kulingana na aina ya shambulizi unalotaka kulijenga . Feisal Salumu alimsoma vyema Kisinda hivyo akaamua kutembea nae kwa kasi huku wakijenga shambulio ambalo linahama box moja kwenda jingine kwenye touch (fairly flat line across the pitch), walifanikiwa kwa kutengeneza goli zuri dakika ya 38. Lakini pia free header ya Sarpong dakika ya 51 pia ni techniques za 4-4-2 au 4-4-1-1 ‘ diamond’ ambapo mawinga kwenye touch lines hucheza kwa kasi ili kuvunja marking zone ya wapingani katika offside trick pia kuruhusu washambuliaji wawili wa kati kujipanga aidha kwa volley crosses au ‘ V’ pass diagonally. Hivi ndivyo Ditram Nchimbi na Sarpong walivyotengeneza goli la pili kwa Yanga mbele ya walinzi wanne wa Aigle . Kasi na maamuzi ya haraka kwa semi volley ya Ditram kutiwa kambani na kichwa cha Sarpong.

Mabadiliko ya wachezaji Yanga SC yaliwaondoa kwenye muhimili wa 4-4-2 na kuingia kwenye 4-5-1 baada ya Sarpong na Ditram kwenda nje na kuingia Haruna Niyonzima na Waziri Junior. Hapa walimu walikuwa wanajaribu mfumo wa kulinda matokeo lakini bado wakiwa na mipango ya kusaka matokeo kwa kutumia viungo wa pembeni au mshambuliaji mmoja wa mbele . Haruna alifanya screening nyingi kumchezesha Waziri ila nadhani bado hajawa sawa na pressure ya timu hiyo . Alikosa nafasi tatu za wazi .

Kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2020-21 ni kizuri na kinatia matumaini kwakuwa kila idara ina key player au players wa kuwazungumzia kwa ubora wao. Save za Shikalo tumeziona , ubora wa Mwamnyeto ni gumzo , eneo la kiungo Kisinda , Feisal , Haruna na Kaseke wanakupa kila sababu ya kuwatazama Yanga kwa jicho la tatu . Sarpong akipata pacha mzuri nadhani atakuwa bora sana kuliko walivyokuwa wanaingiliana kwenye njia na Ditram Nchimbi . Sarpong ni goal machine asiye na mambo mengi uwanjani . Anajua asimame wapi au autafutie njia mpira maeneo gani . Waalimu wa Yanga lazima wamfanyia induction nzuri na viungo ili wavune magoli kupitia yeye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *