October 31, 2020

TUISILA ALIANZISHA YANGA, ATANGULIZIA GOLI MECHI DHIDI AIGLE NOIR

Msomaji wa Yanganews Blog:Bao la dakika ya 41 lililofungwa kistadi na Mcongo Tuisila Kisinda liliamsha shangwe kwenye Uwanja wa Mkapa na mashabiki wengi kuwasha tochi za simu zao wakimaanisha wapinzani wao Aigle Noir ya Burundi wanautafuta mpira kwa tochi.

Tuisila alicheza kwa kiwango bora kipindi cha kwanza akianza katika winga ya kushoto huku kasi yake ikiwa mwiba kwa mabeki wa Aigle Noir.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea AS Vita ya Congo aliwakosha mashabiki wa Yanga kutokana na kasi yake akiwa na mpira huku akipandisha vizuri mashambulizi ya timu yake lakini kubwa lililovutia zaidi ni utulivu wake  na akili pale anapofika eneo la hatari la timu pinzani.

Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi golini kwa Aigle Noir lakini safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Michael Sarpong na Ditram Nchimbi haikuwa makini katika umaliziaji.

Wapinzani wao Aigle Noir nao hawakuwa nyuma kwani walicheza kwa utulivu na kuwa bora katika kupigiana pasi lakini walikutana na ubora wa safu ya kiungo ya Yanga iliyoongozwa na Feisal Salim ‘Fei Toto’ na Mukoko Tunombe.

Dakika 20 za mwanzo Yanga ikionekana ikicheza kwa uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja lakini kadri muda ukivyoenda timu ilicheza kwa uelewano na kufanikiwa kupata bao hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *