October 25, 2020

UWEZO WACHEZAJI YANGA WAMPAGAWISHA MWAMBUSI

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kwa muda mfupi alivyokiona na kukinoa kikosi hicho amegundua wachezaji wengi wapya waliosajiliwa na timu hiyo wana akili na vipaji vikubwa vya soka hivyo timu hiyo itatikisa msimu ujao.

Mwambusi alianza kuinoa timu hiyo Jumatatu ya wiki hii baaada ya kutokuwa na kocha mkuu wa muda mrefu tangu kutimuliwa kwa kocha aliyepita Liuc Eymael kwa kosa la ubaguzi.

Timu hiyo juzi ilimtangaza kocha Zlatko Krmpotic raia wa Serbia kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ambaye atasaidiana na Mwambusi kukiongoza kikosi hicho msimu ujao.

“Baada ya mazoezi ya siku kadhaa hivi sasa tunachoangalia ni kutafuta muunganiko wa wachezaji wapya na wale wa zamani na kadri muda unavyokwenda wanaendelea kuelewana.

“Ukiangalia uongozi chini ya mdhamini GSM wamejitahidi kuleta wachezaji ambao naoina wana akili na vipaji vikubwa hivyo baada ya kupata muunganiko mzuri basi tutapoata Yanga nzuri ambayoitacheza mpira tunaoutarajia,” alisema Mwambusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *