October 25, 2020

MAMBO YAMENOGA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kuhitimisha kilele cha Wiki ya Mwanachi, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yakifungwa na Tuisila Kisinda na Michael Sarpong.

Yanga ilicheza kwa kiwango kizuri licha ya kwamba bado wanahitaji kujifua zaidi ili timu icheze kwa maelewano.

Wachezaji wengi wa Yanga walikuwa wakicheza kwa uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja hasa kipindi cha kwanza lakini muda ulivyoenda walikuwa wanimarika na kucheza kitimu.

Imebaki wiki moja tu kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza Septemba 6 ambapo Yanga itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye dimba la Mkapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *