October 28, 2020

AIGLE NOIR KUMBE NI BALAA HUKO BURUNDI

Msomaji wa Yanganews Blog:Aigle Noir ambayo inacheza na Yanga leo Jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi imetupia mabao 12 katika mechi zao mbili zilizopita Jijini hapa.

Timu hiyo kwenye msimamo wa Ligi ya Burundi ilimaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 48 katika michezo 30.

Katika mechi zao mbili za mwisho kumaliza msimu ilishinda mabao 6-2 dhidi ya Bunjumbura FC lakini baadaye ikawapiga Lieres mabao 6-1. Vital’o ambao walicheza na Simba kwenye Simba Day, walitoka suluhu na Aigles katika ligi.

Katika michezo 30 ya msimu uliopita wa Ligi, Aigle walishinda mechi 13, sare 9 na kupoteza nane.

Bingwa wa Burundi msimu uliopita ni Messager le Ngozi mwenye pointi 64 akifuatiwa na Musongati 56 kwenye nafasi ya pili. Messager kocha wao wa makipa alikuwa Vladmir Niyonkuru ambaye ametua Yanga kama kocha wao mpya wa makipa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *