October 28, 2020

FARID MUSSA ALIANZISHA MAZOEZI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Farid Mussa, jana Agosti 19 ameanza mazoezi na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara msimu 2020/21.

Farid ni ingizo jipya kwa msimu wa 2020/21 amesaini kandarasi ya miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake kwenye Klabu ya CD Tennerife ya Hispania alikokuwa akikipiga awali.

Yanga ilianza mazoezi Agosti 10 mapema kabisa kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria.

Mchezo wa kwanza wa Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara utakuwa dhidi ya Tanzania Prisons, utachezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba sita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *