October 25, 2020

KAIMU KATIBU MKUU AZUNGUMZIA ILIVYOKUWA MIKAKATI KABAMBE YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga  Simon Patrick, amezungumza na chanzo chetu na kueleza mchakato  wa usajili ulipofikia na mipango ya kuukamilisha kwa wakati kabla ya dirisha kufungwa.

“Mchakato wetu wa usajili unakwenda vizuri  tumefanikiwa kuwapata wachezaji wote ambao tulikusudia kuwa nao kwenye kikosi chetu cha msimu ujao, naweza sema tume timiza asilimia 85 ya kuimarisha timu yetu hivyo msimu ujao hakuna kingine zaidi ya kuwazia ubingwa,” alisema Patick.

Kiongozi huyo amedai  uwepo wa beki Bakari Mwamnyeto, kiungo Zawadi Mauya na winga Farid Mussa ukichanganya na Yacoub Songne, Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko na wachezaji wengine wapya na wale waliokuwepo msimu uliopita anaamini utaimarisha jeshi na kwenda kufanya kile walichokikusudia.

Alisema usajili msimu huu wameufanya kwa kuzingatia mambo makubwa mawili ambayo ni kutwaa ubingwa na kurudisha heshima ya timu ambayo imepotea katika misimu mitatu ya hivi karibuni.

“Ukweli tumejinga sababu tulijua matatizo yetu kabla ya msimu uliopita kumalizika ndiyo maana umeona tuliachana na kundi kubwa la wachezaji na kuleta wengine ambao imani yetu wataipigania nembo ya Yanga na kurudisha tabasamu la mashabiki na wanachama wetu ambao wamekuwa wanyonge,” alisema Patrick.

Kiongozi huyo alisema kuwa usajili walioufanya msimu huu unawafanya kutoihofia timu yoyote hapa nchini kwani wamejipanga katika kila idara lengo ni kuhakikisha wanarudisha ufalme wao uliopotea kutokana na changamoto mbalimbali ambazo wamezipitia  ikiwemo za kiuchumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *