October 28, 2020

NI KISHINDO LEO, UJIO TUISLA NA TONOMBE YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kishindo kikubwa kinatarajiwa kusikika kuanzia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hadi mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam wakati Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, wanaoidhamini Klabu ya Yanga atakapotua leo majira ya 7:00 mchana na viungo fundi wawili kutoka DR Congo.

Hersi amekamilisha usajili wa kiungo mkabaji Mukoko Tonombe na winga Tuisila Kisinda kutoka Klabu ya AS Vita ya DR Congo, na leo nyota hao watatua tayari kujiunga na kikosi hicho kinachoendelea na mazoezi katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jijini Dar es Salaam chini ya makocha wasaidizi, Riedoh Berdien na Said Maulid

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *