October 23, 2020

MKURUGENZI GSM APELEKA SHUKRAN KWA MASHABIKI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Yanga leo Agosti 20 wamewapokea majembe yao mawili kutoka Congo ambao ni Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao wataungana na wenzao walioanza mazoezi kujianda na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi kuwapokea na jambo ambalo liliibua furaha kwa mashabiki ni pale walipotengeza kiti na kumbeba juu Makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga, Hersi Sai

Baada ya kupewa mapokezi mazito, mkurugenzi GSM, Enginear Hersi Said kupitia ukurasa wake wa Istagram ameandika “Asanteni wana Yanga kwa mapokezi haya ya kihistoria. Ama hakika huu ni upendo mkubwa sana kwangu na kwa klabu yetu. Sijapenda kubebwa na sikuwa na jinsi ya kukataa kwa hali halisi niliyoikuta pale airport. Zaidi ya yote tuendelee kuijenga klabu yetu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *